JAGUAR AMCHANA TENA PREZZO KUHUSU KUNDI LAKE ALILOANZISHAPrezzo & Cannibal, wakali wanaolikamilisha kundi la MMG.
Moja kati ya Stori kubwa kwenye familia ya burudani 254 kenya kwa sasa, ni kuhusu staa wa single ya kigeugeu msanii Jaguar kuibuka tena na kumzungumzia hasimu wake CMB PREZZO, lakini sasa hivi amefunguka zaidi kuhusu kundi la MMG alilolianzisha Prezzo na kuungana na rappa mwenzake aitwae Cannibal.
Jaguar amesema “ni vizuri lakini mi sipendi jinsi wanavyomkopi Rick Ross na Cannibal kumkopi Lil Wyne, mimi ninaheshima sana kwa Cannibal ila alinistua sana kujiunga na kusainiwa na Prezzo, Cannibal ndio anatakiwa kumsain Prezzo na sio Prezzo kumsain Cannibal, Prezzo anapenda sana kukopi kwenye MMG yeye ni Birdman feki na Cannibali ni Lil Wyne, mimi ni rafiki sana na Cannibal na tunaongea kila siku ila amenishtua sana”Kuhusu BEEF yake na Prezzo, Jaguar amesema “siku hizi naona kama Prezzo ametulia, ameacha yale majigambo yake ya ajabu sasa sijui ni pesa imekwisha, ila namuombea vizuri afanikiwe na siwezi kumuombea aharibikiwe, kama ni muziki anafanya namtakia kila la kheri ila ajue tu always nitakua juu yake kimuziki, simchukii”

No comments: